Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:17

Makubaliano ya magharibi kwa kazi za nyuklia za Tehran yatawezekana;Ayatola Ali


Ayatolá Ali Khamenei, kiongozi wa kidini wa Iran.
Ayatolá Ali Khamenei, kiongozi wa kidini wa Iran.

Miezi kadhaa ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington katika kuokoa makubaliano ya nyuklia na mataifa sita yenye nguvu yamekwama tangu mwezi Septemba huku pande zote mbili zikilaumiana kila mmoja kwa kutoa madai yasiyo na msingi

Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran amesema Jumapili kuwa makubaliano na mataifa ya magharibi kuhusu kazi za nyuklia za Tehran yatawezekana kama miundombinu ya nyuklia ya nchi hiyo itasalia kuwa imara huku kukiwa na mvutano kati ya Tehran na Washington ili kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015.

Miezi kadhaa ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington katika kuokoa makubaliano ya nyuklia na mataifa sita yenye nguvu yamekwama tangu mwezi Septemba huku pande zote mbili zikilaumiana kila mmoja kwa kutoa madai yasiyo na msingi.

Kuidhinishwa kwa Ayatollah Ali Khamenei kunakuja siku chache baada ya Tehran na Washington, kukanusha ripoti kwamba wanakaribia makubaliano ya muda ambapo Tehran itazuia mpango wake wa nyuklia ili kupata nafuu ya vikwazo.

"Hakuna ubaya wowote katika makubaliano hayo na mataifa ya magharibi lakini miundombinu ya sekta yetu ya nyuklia haipaswi kuguswa alisema Khamenei", kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, amekataa kutoa maoni yake kuhusu matamshi ya Khamenei, akisisitiza msimamo wa utawala wa Biden kwamba Marekani haidhamirii kamwe kuiruhusu Iran kupata silaha za nyuklia.

Forum

XS
SM
MD
LG