Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 06:00

Makombora ya Russia yapiga mji ulio karibu na kinu cha nyuklia


Mfanyakazi akisafisha barabara karibu na jengo la utawala la jiji lililokumbwa na mashambulizi ya hivi karibuni katika mzozo wa Ukraine na Russia, huko Donetsk, inayodhibitiwa na Russia Oktoba 16, 2022. REUTERS.
Mfanyakazi akisafisha barabara karibu na jengo la utawala la jiji lililokumbwa na mashambulizi ya hivi karibuni katika mzozo wa Ukraine na Russia, huko Donetsk, inayodhibitiwa na Russia Oktoba 16, 2022. REUTERS.

Milio ya roketi ilisababisha uharibifu mwingine nchini Ukraine Jumapili, huku maafisa wanaounga mkono Kremlin wakiilaumu Kyiv kwa shambulio lililoikumba ofisi ya meya katika mji wa Donetsk unaodhibitiwa na watu waliojitenga.

Wakati hayo yakijiri mamlaka nchini Ukraine ilisema kuwa makombora ya Russia yalipiga mji ulio karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, na kujeruhi watu sita

Jengo la meya huko Donetsk, sehemu ya eneo la Ukraine ambalo Russia ilidai kuwa ni lake hivi karibuni liliharibiwa vibaya, likiwa na safu za madirisha yaliyolipuliwa na dari iliyoporomoka kwa kiasi. Magari yaliokuwa karibu yaliteketezwa.

Hakukuwa na ripoti za mara moja za majeruhi. Serikali ya Kyiv haikudai kuhusika na shambulio hilo au kutoa maoni yake juu yake.

Ukraine ilisema shambulio hilo karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, kando na majeraha, pia liliharibu njia tano za umeme, mabomba ya gesi, na biashara kadhaa za kiraia na majengo ya makazi.

Russia na Ukraine zimeshutumiwa mara kwa mara kwa kurusha risasi karibu na mtambo huo. Unadhibitiwa na Russiai lakini unaendelea kuendeshwa na mafundi wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG