Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:17

Mazingira ya njaa katika pembe ya Afrika


Mtoto wa Kisomali aliyekondeana kutokana na baa la njaa
Mtoto wa Kisomali aliyekondeana kutokana na baa la njaa

Katika mwanzo wa makala yetu maalum juu ya ukame na njaa katika Pembe ya Afrika tunatupia jicho historia na tatizo la baa la njaa kwa ujumla katika ukanda huo.

Swala la ukame na njaa si geni kwa bara la Afrika, lakini athari zake ni kubwa. Kwa wakati huu Pembe ya Afrika imeathiriwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 60.

Mnamo Julai 20, Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi njaa katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa Somalia, baa kali la njaa kuwahi kukumba taifa hilo katika muda wa miaka 20. Kenya, Ethiopia na Djibouti pia zimeathiriwa sana na ukame na njaa na maelfu ya watu wanahitaji misaada ya dharura kuokoa maisha.

Lakini nini maana ya njaa? Umoja wa Mataifa unaelezea njaa pale ambapo utapia mlo unazidi kiwango cha asili mia 30; pale ambapo watu wawili kati ya elfu 10 hufa kila siku kutokana na njaa, na pale ambapo kunatokea uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu.

Tukiangalia historia, Somalia ilikumbwa na baa la njaa kati ya mwaka wa ’91 na ’92 na kuuwa watu laki tatu. Mbunge wa serikali ya mpito ya Somalia Hussein Bantu, anasema katika maisha yake, hajawahi kushuhudia kiwango cha njaa anachoshuhudia hivi leo nchini Somalia.

Lakini wengi wanapoona picha za watoto waliosononeshwa na njaa, waliokonda na kukondeana kutoka Somalia na maeneo ya kaskazini mwa Kenya, hukumbuka picha za ukame, maafa na njaa iliyokumba Ethiopia miaka ya ’84 na 85. Baa hilo la njaa liliuwa raia wa Ethiopia wapatao milioni moja na maelfu ya wengine mwaka wa 1974.

Kote duniani,watu wanashuhudia wimbi la wakimbizi wa Somalia hivi sasa walioathiriwa zaidi na njaa. Pamoja na hayo tatizo la makundi ya kigaidi na wanamgambo nchini mwao, na serikali isiyo thabiti ya muda.

Lakini je endapo jamii ya kimataifa ingeliingilia kati mzozo wa kisiasa wa Somalia mapema na kusaidia kuunda serikali thabiti inayojenga mifumo na taifa thabiti matatizo haya yanayotoa wengi machozi leo yangelikuwepo?

Mbunge wa serikali ya mpito ya Somalia bwana Bantu anasema dunia, iliipuzilia mbali zamani nchi yake ya Somalia. Nchini Kenya, kambi za Daadab na Kakuma kwa miaka mingi zimepokea wakimbizi wa Somalia na wengine kutoka Sudan na nchi zingine.

Wanawake wakitafuta maji karibu na kambi ya Dadaab
Wanawake wakitafuta maji karibu na kambi ya Dadaab

Lakini tatizo la sasa la ukame limeshuhudia kufurika kwa wakimbizi hao, ambao wamelazimisha shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR kuomba serikali ya Kenya kuruhusu kujengwe kambi ya tatu.

Na japo serikali ya Kenya ilisita, hatimaye ilikubali wakimbizi wa wa njaa wa Somalia wahudumiwe nchini humo. Msemaji wa shirika hilo la UNHCR mjini Nairobi Emmanuel Nyabera anakiri kuwa kambi ya wakimbizi ya Daadab haitoshi kuhudumia wimbi la wakimbizi wa Somalia wanaoingia nchini Kenya.

Ardhi iliyokauka kutokana na ukame kaskazini mashariki ya Kenya
Ardhi iliyokauka kutokana na ukame kaskazini mashariki ya Kenya

Kutokana na ukame katika pembe ya Afrika na hata Afrika Mashariki, watu wengi wamelazimika kuuza mifugo yao kwa sababu hawana chakula kwa mifugo hao. Wengi hatimaye kufa na hii ni hasara maradufu kwa wenye mifugo ambao pia hawana chakula.

Jamii ya wakenya wanaoishi katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya pia ambapo kambizi za wakimbizi zimejengwa wanaelezea hofu yao juu ya ongezeko la uhalifu, wengine wakishuku kuwa kundi la kigaidi la al-shabab litapata fursa na njia rahisi kuingia nchini humo.

Na ingawa shirika la wakimbizi la Umoja wa mataifa limeanza ujenzi wa kambi ya tatu kwa jina IFO extension, kundi la madaktari wasio na mipaka wanasema kambi hiyo haipo tayari kutoa huduma zinazostahiki kwa wakimbizi hao.

Tatizo la wakimbizi pia limezusha hofu juu ya uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa bei ya vyakula na na hata nyumba za kukodi katika maeneo yaliyo karibu na kambi za wakimbizi.

Na ingawa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yameanza kutoa misaada kwa waathiriwa wa njaa, hali katika Pembe ya Afrika inaendelea kuwa kitisho hasa kwa watoto na kina mama.Katika majuma ya hivi karibuni, wakimbizi wa Somalia waliokimbilia kambi za Kenya wamefika wakiwa wadhoofu wa afya, na wengine wameaga dunia.

Wakimbizi katika kambi ya Dadaab, Kenya
Wakimbizi katika kambi ya Dadaab, Kenya

Wengi wanatembea kwa siku hata wiki na hatima yao ni mchanganyiko, wengine na wanapona na wengine watupa mkono wa buriani .Umoja wa Mataifa unaonya hali itaendelea kuwa tete katika maeneo ya kusini mwa Somalia, na hata kaskazini mwa Kenya.

Ama kwa kweli hizi sio habari tu unazosikia zikakupita, hata wewe, una fursa ya kuchangia, kusaidia binaadamu mwenzako anayekabiliwa na tishio la kufa njaa bila kujali misingi yake ya kidni, utaifa wake au rangi yake.

<table>

<tbody>

<tr>

<p><strong><sub>Mdundiko</sub></strong><br /><br />

<object id="single1" width="295" height="24" data="http://www.voanews.com/MediaAssets2/player/jw/player.swf" type="application/x-shockwave-flash">

<param name="data" value="http://www.voanews.com/MediaAssets2/player/jw/player.swf" />

<param name="name" value="single1" />

<param name="allowfullscreen" value="true" />

<param name="allowscriptaccess" value="always" />

<param name="wmode" value="transparent" />

<param name="flashvars" value="file= http://www.voanews.com/MediaAssets2/swahili/dalet/Mdundiko.Mp3&backcolor=7FA3BD&frontcolor=FFFFFF" />

<param name="src" value="http://www.voanews.com/MediaAssets2/player/jw/player.swf" />

<param name="bgcolor" value="#ffffff" />

</object>

</p>

</tr>

</tbody>

</table>
XS
SM
MD
LG