Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:39

Maisha magumu baada ya Septemba 11


Maadhimishi ya Septemba 11 2011 mjini New York
Maadhimishi ya Septemba 11 2011 mjini New York

Uchunguzi wa maoni na jarida la Time umebaini kuwa asilimia 71 ya wamarekani wanaiona Marekani ikiwa katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa muongo mmoja uliopita.

Uchunguzi huo uliofanywa na taasisi ya Gallup unaonyesha pia asilimia 88 ya wale waliohojiwa hawaridhishwi na mwelekeo wa nchi.

Maoni ya Wamarekani

Mzima moto Derek Spector wa huko Arlington, Virginia hana tatizo kukumbuka mahali alipokuwa September 11 mwaka 2001.

“Kwa kweli tulipelekwa Rosslyn ambako kulikuwa na moto, na wakati tukijitayarisha kuondoka huko, tulisikia ndege imeanguka huko Pentagon. Na tulipokuwa tunaingia kwenye kituo cha zima moto tulisikia mshtuko huo”.

Spector alikuwa miongoni mwa wazima moto wa kwanza kujibu shambulizi la Pentagon.

Hivi karibuni alishiriki katika kumbukumbu ya kuendesha piki piki kuwakumbuka wale waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo na wakijumuika na polisi na zima moto ambao waliwajibika siku hiyo.

Specter alisaidia kupandisha kile kinachoelezewa bendera ya uzalendo, bendera kubwa ya marekani ambayo inapeperushwa katika mataifa yote 50 kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha yao September 11 na wanajeshi ambao wamepigana vita nchini Afghanistan na Iraq.

“Nadhani inaashiria kila kitu ambacho ni kizuri katika nchi hii. Siasa iweke kando, viondoe vyama, bado sisi ni wamarekani, bado tunaithamini nchi hii, bila kujali tunachosema au tunachofanya. Ndani ya mioyo yetu bado tunaiamini nchi hii na tunaithamini sana nchi yetu”.

Juhudi hizi ndogo kwa umoja wa kitaifa zinakuja wakati muafaka, anasema mkusanyaji maoni na mtaalamu wa siasa, Mark Penn.

“Ni takriban miaka saba hivi sasa ambapo watu wanadhani kwamba mambo humu nchini yako kwenye njia isiyo sahihi na watu wengi wanadhani kwamba huu umekuwa si muongo mzuri kwa marekani tangu September 11”.

Mchunguzi wa maoni Mark Penn anasema wamarekani wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa ikionekana hapo kabla.

“Kwa ndani kuna imani kubwa kamba hii ni nchi nzuri na ingawaje huenda inapitia kipindi kigumu sana, bado kuna dhana kuwa thamini za nchi ni kubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali”.

Miongoni mwa wale wanaohamasisha ujumbe wa mshikamano ni mfanyakazi wa zima moto huko new york, joe torillo. Alikimbia haraka kwenda kwenye jengo la World Trade Center hapo September 11 na alifanikiwa kunusurika wakati majengo ya Twin Towers yalipoanguka.

“Nimekuwa msemaji wa hiyo bendera ya uzalendo na utashi wangu au azma yangu baada ya kuchimbuliwa kutoka upande wa kusini wa jengo mojawapo na hivi sasa naishi maisha yangu kwa kuhamasisha Marekani iliyoungana, kwa sababu siku ya September 1, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya changamoto kubwa hapo ndiyo unajifahamu na kujua nguvu yetu”.

Torillo alizungumzia kuhusu kile anachokijua kuhusu September 11 kote nchini na kuelezea kuhusu bendera ya uzalendo ambayo hivi sasa inapepea katika majimbo yote 50. Katika maadhimisho haya ya kumi ya mashambulizi ya kigaidi, bendera hiyo itapeperushwa katika maeneo matatu ambayo yalishambuliwa mwaka 2001 – World Trade Center, eneo ambalo hivi sasa linajulikana kama Ground Zero, huko New York, huko Pentagon katika jimbo la Virginia na huko Shanksville katika jimbo ya Pennyslvania, ambako moja ya ndege zilizotekwa nyara ilianguka.

XS
SM
MD
LG