Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:51

Mahakama kuu ya Tanzania yamaliza mzozo wa mita 200


Mahakama kuu ya Tanzania iliamua kutoruhusu mikusanyiko ya watu umbali wa mita 200.
Mahakama kuu ya Tanzania iliamua kutoruhusu mikusanyiko ya watu umbali wa mita 200.

Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Dar Es Salaam, Alhamis iliamua kutoruhusu mikutano wala mikusanyiko yeyote ya watu umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika hukumu ya shauri la kikatiba lililofunguliwa na mwananchi mmoja hivi karibuni.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa shauku na watanzania ilifuatia shauri hilo la kikatiba lililofunguliwa na mgombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, alipoiomba mahakama kutoa tafsiri ya kifungu cha sheria namba 104 kifungu kidogo cha 1,sura ya 343, akiomba mahakama iangalie maana ya kifungu hicho cha watu kuweza kukaa mita 200 kutoka umbali wa kituo cha kupiga kura.

Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji watatu lililokuwa linaongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo, jaji Lugano Mwamdambo , alisema mahakama hiyo katika tafsiri yake, ilisema, sheria iko wazi na bayana na kwamba inakataza mikutano, bila kujali umbali na kwamba tafsiri ya sheria namba 72 inaeleza watu gani wanapaswa kuwepo sehemu ya kuhesabia kura na kwamba ambaye hakutajwa hatakiwi kuwepo eneo hilo.

Akisisitiza tafsiri hiyo, kiongozi wa jopo la majaji hao,Jaji Sakieti Kihiyo, alisema,sheria inakataza pia mikusanyiko, uwepo wa nembo, bendera ama alama yoyote ya chama umbali wowote katika siku hiyo ya uchaguzi.

Mahakama kuu ya Tanzania yakamilisha mzozo wa mita 200
Mahakama kuu ya Tanzania yakamilisha mzozo wa mita 200



Baada ya tafsiri hiyo kutolewa na mahama kuu kanda ya Dar Es Salaam pande zote mbili yaani walalamikiwa ambao ni mwanasheria mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiwakilishwa na naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Dokta Tulia Jackson, katika nyakati tofauti mahakamani hapo walizungumzia walivyopokea tafsiri hiyo.

Wakili Peter Kibatala, aliyemwakilisha mlalamikaji, alisema,wamepokea uamuzi huo wa mahaka kwa heshima lakini watakata rufaa.

Watanzania wanatarajiwa kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kumchaguwa rais, wabunge na madiwani, katika uchaguzi ambao vyama vinane vimesimamisha wagombea wa urais.

XS
SM
MD
LG