Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:46

Mahakama Kenya imemuachia huru mhubiri Deya kwa kukosa ushahidi wa kutosha


Mfano wa makanisa ambayo mhubiri Gilbert Deya aliyaongoza huko London hadi mji wa Manchester
Mfano wa makanisa ambayo mhubiri Gilbert Deya aliyaongoza huko London hadi mji wa Manchester

Gilbert Deya, fundi muashi aliyehamia London kutoka Kenya katikati ya miaka ya 90 alituhumiwa kuiba watoto watano kati ya mwaka 1999 na 2004 ili kufutilia mbali madai yake. Hakimu mwandamizi Robison Ondieki alimkuta hana hatia mwanamme huyo

Mahakama moja nchini Kenya imemwachilia huru mhubiri mmoja mwenye tabia yenye utata ambaye anadai anaweza kuwasaidia wanandoa kupata mimba kwa njia ya maombi, “watoto wa miujiza”, ikielezea kutokuwepo na ushahidi wa kutoka kwa waendesha mashtaka.

Gilbert Deya, fundi muashi aliyehamia London kutoka Kenya katikati ya miaka ya 90 alituhumiwa kuiba watoto watano kati ya mwaka 1999 na 2004 ili kufutilia mbali madai yake. Hakimu mwandamizi Robison Ondieki alimkuta hana hatia mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 86 na kutoa maamuzi kwamba upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kumhusisha Deya na mashtaka hayo.

Mhubiri huyo, ambaye anaongoza Gilbert Deya Ministries alikuwa na makanisa katika miji ya London, Birmingham, Nottingham, Liverpool na Manchester, alifukuzwa kutoka Uingereza kwenda Kenya mwaka 2017 kufuatia mapambano ya kisheria vya muongo mmoja ili kubaki Uingereza.

Deya na mkewe Mary walidai kuwa maombi yao yanaweza kuona wanawake wasio na uwezo wa kushika mimba na hata baada ya ukomo wa hedhi kupata mimba ndani ya kipindi cha miezi minne, na bila kufanya tendo la ndoa.

Forum

XS
SM
MD
LG