Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:04

Mahakama ya Rufaa ya Kenya yasitisha amri ya kutotumika kwa sheria mpya ya fedha Kenya


Maandamano ya kupinga sheria mpya ya fedha mjini Nairobi. Juni 6, 2023.
Maandamano ya kupinga sheria mpya ya fedha mjini Nairobi. Juni 6, 2023.

Mahakama ya Rufaa ya Kenya imebatilisha amri iliyotolewa mwezi uliopita ya kusimamisha kwa muda utekelezwaji wa sheria mpya ya fedha ya 2023, baada ya waziri wa Fedha Prof Njuguna Ndung’u kusema kwamba serikali inapoteza nusu bilioni kila siku kutokana na hatua hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Ijumaa, jopo la majaji watatu wa Rufaa limeondoa amri hiyo iliyowekwa Juni 30, wakati rufaa iliyowasilishwa na waziri Ndung’u ikisubiriwa.

Awali Ndung’u kupitia kwa mwanasheria mkuu wa Kenya, Justin Muturi aliwasilisha rufaa mahakamani akisema kwamba serikali huenda ikapoteza takriban shilingi bilioni 211, ndani ya mwaka huu wa kifedha iwapo sheria hiyo itasitishwa.

Waziri huyo alisema kwamba bila kutekelezwa kwa sheria hiyo, serikali ya Kenya Kwanza haitaweza kutekeleza majukumu yake ya bajeti ya mwaka 2023/24 kama ilivyopangwa. Majaji Mohammed Warsame, Kathurima M’Inoti na Hellen Omondi wamesema kwamba mswada wa fedha una siku 90 kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa kifedha.

Forum

XS
SM
MD
LG