Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 01:09

Rais achukua rasmi hatamu za uongozi


Rais John Magufuli akikagua gwaride la kijeshi wakati wa sherehe za kuapishwa kwake kwenye uwanja wa michezo wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Rais John Magufuli akikagua gwaride la kijeshi wakati wa sherehe za kuapishwa kwake kwenye uwanja wa michezo wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Rais mpya wa Tanzania, John Magufuli ameapishwa Alhamisi kuchukua uongozi wa nchi kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Rais Magufuli anachukua wadhifa huu huku wananchi wa Tanzania wakiwa na matumaini kuwa atatekeleza ahadi ambazo amezitoa wakati wa kampeni za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kufungua milango ya ajira kwa vijana, kukabiliana na rushwa kwa nguvu zaidi na kuhakikisha serikali yake inaboresha miundo mbinu ya nchi ambayo inachangia katika uchumi wa taifa.

Katika hotuba fupi aliyoitoa baada ya kuapishwa ameahidi kutekeleza ahadi alizozitoa .

Lakini mchambuzi wa masuala ya kisiasa Mwalimu Bashiru Ally wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ameainisha changamoto mbili kubwa ambazo hazihitaji kusubiri muda mrefu, suala la mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar na kupatikana kwa katiba mpya ya Tanzania.

Katika mahojiano na Idhaa hii amezungumzia kwa kina changamoto hizo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:08:37 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais mpya ambaye ana umri wa miaka 56 amehudumu katika serikali katika nafasi ya uwaziri kwa takriban miaka 15, kwa muda mrefu akishughulikia masuala ya ujenzi ambapo kazi kubwa ilihusisha ujenzi wa barabara mbali mbali nchini humo.

XS
SM
MD
LG