Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:56

Mafuriko ya Somalia yapelekea maelfu kuhama makwao


Watu wakitembea kwenye maji ya mafuriko Somalia. Picha ya maktaba.
Watu wakitembea kwenye maji ya mafuriko Somalia. Picha ya maktaba.

Mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Somalia yamepelekea zaidi ya watu 113,000 kuhama makwao, huku wengine maelfu wakiathiriwa na hali hiyo, kulingana na ofisi ya UN ya kuratibu masuala ya kibinadamu, UNOCHA.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban watu 10 wamekufa kufuatia mvua hizo, wakati serikali ikitangaza hali ya dharura, Idara ya kitaifa ya dharura ya Somalia imesema kupitia ukurasa wake wa X, uliojulikana kama Twitter.

Mvua hizo zimekuja mwaka mmoja baada ya taifa hilo la pembe ya Afrika kukumbwa na ukame mbaya zaidi ndani ya miongo minne, wakati pia kukiwa na ghasia, pamoja na kupanda kwa bei za vyakula kutokana na vita vya Ukraine,na kwa hivyo kusababisha vifo vya hadi watu 43,000 nchini humo, kulingana na UN.

Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Decemba umeshuhudia mvua nyingi kwenye majimbo ya Puntland, Galmudug, South West, na Hirchabelle, pamoja na maeneo karibu na mto Juba, kwenye jimbo la Jubbaland, shirika la OCHA likisema ni kutokana na hali ya El Nino.

Mapema mwaka huu, mafuriko yalisababisha robo milioni ya watu kuhama makwao baada ya mto Shabelle kuvinja kingo zake katikati mwa Somalia na kusomba nyumba katika mji wa Beledweyne. Mashirika ya kutoa misaada pamoja na wanasayansi wameonya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni miongoni ya sababu zinazopelelea majanga ya kibinadamu, wakati waathirika wakiwa ni wale ambao hawazalishi gesi nyingi ya carbon kutokana na viwanda.

Forum

XS
SM
MD
LG