Mafuriko makubwa yaliikumba Mauritius siku ya Jumatatu wakati kimbunga cha hatari cha kitropiki kilipokuwa kinakaribia katika taifa hilo la kisiwa cha Bahari ya Hindi baada ya kukumba eneo la Reunion la Ufaransa.
Picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya eneo hilo katika kisiwa kidogo cha Paradise zilionyesha magari yakizama au kuchukuliwa na maji yaliyofurika mitaani. Uwanja wa ndege wa kimataifa ulitangaza kuwa utafungwa kuanzia saa kumi na nusu jioni kwa saa za huko hadi itakapotolewa taarifa zaidi wakati mabenki, ofisi za serikali na biashara nyingine za binafsi zikifunga ofisi na kuwarudisha wafanyakazi majumbani.
Idara ya Hali ya Hewa ya Mauritius (MMS) imesema katika taarifa yake kwamba tahadhari ya kimbunga cha daraja la tatu, kati ya viwango vinne imeanza kutumika na kuwashauri wananchi kukaa katika sehemu salama, huku hali ya mvua ikitarajiwa katika saa zijazo.
Forum