Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 17:06
VOA Direct Packages

Maelfu ya wafanyakazi wa Tunisia washiriki kwenye maandamano ya kupinga utawala


Baadhi ya waandamanaji waliojitokeza kwenye barabara za miji ya Tunisia Jumamosi
Baadhi ya waandamanaji waliojitokeza kwenye barabara za miji ya Tunisia Jumamosi

Maelfu ya wafanyakazi kutoka umoja wa chama   wafanyakazi nchini  Tunisia  UGTT, Jumamosi wameingia mitaani  katika miji 8 nchini humo, kulalamikia sera za rais Kais Saied.

Walioshiriki wanamshutumu Saied kwa sera zake, ambapo anajaribu kukandamiza uhuru wao, zikiwemo haki za kuwa wanachama wa umoja huo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters maandamano ya hayo ni mwendelezo wa mivutano kati ya umoja wao na utawala wa Saied, kufuatia kukamatwa kwa watu wanaoipinga serikali wakiwemo wanasiasa, wanahabari, majaji wawili pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa UGTT.

Ukamataji huo umezua wasiwasi wa kuendelea kwa msako dhidi ya wapinzani, na kupelekea ofisi ya umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kuomba kuachiliwa mara moja wa wale waliozuiliwa. Mmoja wa viongozi wa UGTT Othman Jalouli wakati akihutubia waandamanaji amesema kwamba serikali ya Saied ina nia ya kuzima sauti ya umoja wao. Baadhi ya miji iliyoshiriki kwenye maandamano hayo ni pamoja na Jendouba, Tozeur, Monastir, Bizerte, Kasserine, Kairouan na Nabeul. Maandamano zaidi yamepangwa katika siku zijazo kwenye miji zaidi.

XS
SM
MD
LG