Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:49

Madagascar yatoa amri ya kutotoka nje kwenye mkesha wa uchaguzi


Polisi wa kuzuia gasia wakishika doria kwenye mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, baadha ya ghasia wakati wa kampeni.
Polisi wa kuzuia gasia wakishika doria kwenye mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, baadha ya ghasia wakati wa kampeni.

Madagascar Jumatano imetoa amri ya kutotoka nje nyakati za usiku ukiwa mkesha wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliozuwa utata kufuatia zaidi ya wiki 6 za maandamano ambayo mamlaka imekuwa ikutimia gesi ya kutoa machozi pamoja na ghasia kuyatuliza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya wagombea 10 kati ya 12 wa upinzani kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, wakidai kuwa rais Andry Rajoelina hafai kugombea, na kwa hivyo kuwashauri wafuasi wao kutoshiriki uchaguzi huo wa Alhamsini, kwenye kisiwa hicho kilichoko katika bahari Hindi.

“Ni lazima tuimarishe usalama ili kuzuia matukio kufanyika,” amesema mkuu wa polisi Angelo Ravelonarivo. Miongoni mwa wagombea wanaosusia uchaguzi huo ni pamoja na Marc Ravalomanana aliyewahi kuwa rais wa taifa hilo.

Kando na baadhi ya vyama kususia uchaguzi huo, shirika la makanisa manne makubwa ya Madagascar pia limetangaza leo kwamba halitatambua uchaguzi huo, likidai hali ya kisiasa iliyopo siyo mwafaka, pamoja na ukosefu wa maadili. Hata hivyo kampeni za Rajoelina hazikuonekana kuathiriwa na tangazo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG