Poland, Hungary na Slovakia hapo awali zilitangaza marufuku ya uagizaji wa baadhi ya bidhaa kutoka Ukraine, huku baadhi ya mataifa ya Ulaya ya kati na mashariki yakisema kuwa huenda yakafuata nyayo. Mataifa hayo matatu yanadai kuwa bei za chini za bidhaa za kilimo kutoka Ukraine zinawaumiza wakulima wa ndani.
Poland na Hungary walitangaza marufuku hiyo mwishoni mwa wiki wakisema kwamba itadumu hadi Juni 30. Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kwamba marufuku ya Slovakia itaanza kufanya kazi Jumatano. Msemaji wa kitengo cha utendaji katika EU amesema kwamba ni lazima suluhisho lipatikane ambalo linaheshimu muundo wa kisheria wa EU shirika la habari la Assciated Press limeripoti.
Marufuku hiyo inakuja wakati Russia inaonya kuwa huenda isiendeleze mkataba wa nafaka wa Black Sea unaoruhusu usafiri wa meli za nafaka kutoka Ukraine, na utakaomalizika Mei 18