Maafisa wa usalama nchini Kenya wanasema maafisa wawili wa polisi wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa wakati gari waliyokuwa wakisafiria ilikanyaga kilipuzi kwenye barabara ya Garissa na Dadaab, katika kaunti ya Garissa. Maafisa hao wamekataa kujibu ombi la VOA kutoa maoni yao.
Mbunge wa Dadaab Farah Maalim katika kaunti ya Garissa amesema “njia ya kukabiliana na al-Shabaab siyo kutumia mbinu za kijeshi bali ni kukabiliana nao kwa kuwafuatilia na kuwakamata mmoja mmoja.” Tukio hilo limetokea Ijumaa asubuhi na limekuja kiasi cha wiki moja tu baada ya maafisa watatu wa polisi kutoka Kitengo cha Doria cha Mpakani kuuawa katika eneo hilo hilo wakati gari lao lilipolipuliwa.
Kundi la kiislamu katika siku zilizopita kutokana na mashambulizi katika miji kadhaa ya Kenya ikiwa ni jaribio la Kenya kuondoa wanajeshi wake kutoka kikosi cha ulinzi wa amani kinachoongozwa na Umoja wa Afrika nchini Afrika.