Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 11:55

Libya yafunga kinu muhimu cha mafuta kutokana na maandamano


Picha ya kinu cha mafuta cha El Sharara, Libya. Picha ya Desemba 3, 2014.
Picha ya kinu cha mafuta cha El Sharara, Libya. Picha ya Desemba 3, 2014.

Shirika la kitaifa la mafuta la Libya, NOC, Jumapili limetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa shuguli za uchimbaji mafuta kwenye kinu cha Sharara, chenye uwezo wa kuzalisha mapipa 300,000 ya mafuta kila siku.

Hatua hiyo ni kutokana na maandamano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Uzalishaji wa mafuta wa Libya umekuwa ukiathiriwa mara kwa mara kwa zaidi ya muongo mmoja sasa tangu 2011, baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi, kufuatia mapinduzi yalioungwa mkono na NATO.

NOC kupitia taarifa limesema kwamba kufungwa kwa kinu cha Sharara kutasitisha upelekaji wa mafuta ghafi kuelekea kituo cha kuhifadhia cha Zawiya. Sharara ni moja ya vinu vikubwa zaidi vya mafuta nchini Libya, na kimekuwa kikilengwa mara kwa mara kwenye maandamano kutokana na sababu za kisiasa.

Kinu hicho kinapatikana kwenye eneo la Murzuq, lililopo kusini mashariki mwa Libya, wakati kikiendeshwa na NOC, kupitia makampuni ya mafuta ya Repsol kutoka Uhispania, Total ya Ufaransa, OMV ya Australia, na Equinor ya Norway.

Forum

XS
SM
MD
LG