Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 13:08

Kombe la Dunia; Morocco yaweka historia imeifunga Portugal 1-0


Kikosi cha timu ya Morocco kikifurahia ushindi wake uliotoa fursa ya kusonga mbele kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar
Kikosi cha timu ya Morocco kikifurahia ushindi wake uliotoa fursa ya kusonga mbele kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar

Bao la ushindi lilifungwa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza wakati Youssef En-Nesyri alipoteleza na kushinda kwa kichwa krosi iliyopigwa na Yahya Attiat-Allah. Kipa wa Portugal Diogo Costa alijaribu kumzuia En-Nesyri kwa krosi lakini En-Nesyri alimruka kila mmoja na kuutumbukiza mpira wavuni

Morocco imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kusonga mbele katika nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Portugal siku ya Jumamosi.

Bao la ushindi lilifungwa katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza wakati Youssef En-Nesyri alipoteleza na kushinda kwa kichwa krosi iliyopigwa na Yahya Attiat-Allah. Kipa wa Portugal Diogo Costa alijaribu kumzuia En-Nesyri kwa krosi lakini En-Nesyri alimruka kila mmoja na kuutumbukiza mpira wavuni.

Hatua ya Morocco kutinga nusu fainali huenda inamaliza nafasi ya Cristiano Ronaldo kushinda Kombe la Dunia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 alianzia kwenye benchi kwa mechi ya pili mfululizo na aliingia dakika chache tu kipindi cha pili. Nafasi yake nzuri ya kufunga mabao ilikuja katika dakika ya 91 wakati Ronaldo alipopata fursa nzuri ya kulenga goli akiwa kati ya mabeki wawili wa Morocco. Lakini mkwaju wake uliokolwa na Yassine Bounou.

Morocco iliifunga Portugal mabao 3-1 mwaka 1986 na kuliondoa taifa hilo la Ulaya katika hatua ya makundi. Portugal ililipiza kisasi mnamo 2018 kwa bao la dakika ya nne la Ronaldo na kushinda 1-0. Cristiano Ronaldo amefunga mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia (8) bila kufunga bao hata moja lkatika hatua ya mtoano.

Jiji la Doha lasheherekea

Jiji la Doha limegubikwa na bendera nyekundu na honi za barabarani a washabiki so tu wa Morocco bali wote kutoka Afrika na mashariki ya kati wanaunga mkono timu hii.

Watu wengi wamemiminika katika maeneo ya kati kati ya jiji kusheherekea ushindi huo wa bara la Afrika na hata mamlaka imeongeza muda wa usafiri wa treni ambao kwa kawaida unafungwa saa tisa alfajiri ila kwa siku hii wameongeza hadi saa 11 alfajiri ili kuwapa nafasi wananchi kuendelea kubaki nje na kusheherekea.

Wakati huo huo pia kumetenegenezwa taa zinazoelea angani kwa njia ya drone za kupendezesha na kuwashangilia Morocco.

Mshabiki Ahmed Ally kutoka Kenya anasema hii ni heshima kubwa kwa bara la Afrika na leo anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa mwafrika baada ya ushindi huu.

Timu tatu za mwisho za Kiafrika kufika robo fainali ya Kombe la Dunia zilitoka kwa maumivu makubwa zaidi. Cameroon mwaka 1990 walipoteza 3-2, dhidi ya Uingereza baada ya muda wa ziada kwa penalti ya pili ya Gary Lineker katika dakika ya 105; Senegal mwaka 2002 walikuwa walipoteza, 1-0, kwa Uturuki kwa bao la mchezaji wa akiba Ilhan Mansiz dakika ya 94; na Ghana walipoteza kwa mikwaju ya penalti kupitia udanganyifu wa Uruguay wakati Luis Suárez alipotoa mpira muda mfupi kabla ya penalti hizo kwa mkono na Ghana walipewa penalti lakini walikosa mkwaju huo wa penalti.

XS
SM
MD
LG