Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:27

Gari lauwa mmoja, kujeruhi watatu Russia


Ramani ya mji wa Sochi
Ramani ya mji wa Sochi

Mtu aliyekuwa anatembea kwa miguu aliuwawa na wengine watatu kujeruhiwa Jumatano katika mji wa Sochi panapochezwa Kombe la Dunia, wakati gari moja lilipoacha njia na kuelekea kwenye eneo la watembea kwa miguu na kusababisha ajali.

Polisi wameiambia Reuters dereva wa gari hilo alipitiwa na usingizi wakati gari likienda mbio katika moja ya barabara kuu kabla ya kukatiza laini mbili barabarani na kuwagonga watembea kwa miguu hao.

Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea takriban kilomita 45 kutoka uwanja wa mpira wa Sochi, mmoja kati ya miji kumi na moja ambako Kombe la Dunia linachezwa.

Vyombo vya dola viliahidi kuwepo viwanja salama kwa ajili ya mechi hizo, lakini mwezi uliopita dereva wa taxi aliingiza gari hilo katikati ya umati wa watu karibu na eneo la Red Square, Moscow, na kuwajeruhi watu saba.

XS
SM
MD
LG