Ripoti za karibuni kutoka kituo cha kitaifa cha majanga, tawi la Miami zimesema kwamba Otis kipo takriban kilomita 10 kusini mwa mji maarufu wa mapumziko wa Acapulco, kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 270 kwa saa, ambayo ni juu zaidi na wenye uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa.
Idara ya kitaifa ya hali ya hewa imetoa ilani kwa jimbo la Guerrero, ambako uko mji wa Acapulco, pamoja na jimbo jirani la Oaxaca. Watabiri wa hali ya hewa wamesema kwamba kimbunga hicho huenda kikasababisha mvua za kuanzia centimita 20 hadi 40 kwenye majimbo hayo. Otis pia huenda kikasababisha mafuriko hatari kwenye ufukwe, pamoja na mawimbi makubwa.
Forum