Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:04

Kiir na Machar watakutana tena Ethiopia wiki ijayo


Riek Machar (L) na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Riek Machar (L) na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar watakutana Juni 20 mjini Addis Ababa kwa mazungumzo ya ana kwa ana kama sehemu ya juhudi za upatanishi zinazofanywa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kuweza kupatikana mkataba wa amani kati ya wawili hao.

Msemaji wa Machar alisema katika taarifa kwamba “kundi linaukaribisha mwaliko huu, itachukua muda mrefu kujenga uaminifu katika utaratibu wa amani”. Hakuna majibu yeyote yaliyosikika kutoka serikali ya Sudan Kusini au kutoka IGAD. Hata hivyo msemaji wa Kiir, Ateny Wek Ateny aliuita mwaliko huo ni hatua muhimu.

Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar.
Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar.

Wakati huo huo msemaji wa upinzani wa SPLM-In, Mabior Garang alithibitisha katika kipindi cha “South Sudan in Focus” cha VOA kwamba Machar atasafiri kutoka nchini Afrika kusini kwenda Ethiopia kwa ajili ya mkutano huo. Garang alisema ajenda ya mkutano bado haijajulikana lakini viongozi hao wawili wanatarajiwa kutanzua baadhi ya masuala yenye utata yanayozuia njia ya kuelekea amani huko Sudan Kusini.

Mkutano wa Addis Ababa unatarajiwa kuongozwa na jumuia ya kikanda ya Afrika mashariki-IGAD ambayo imekua mpatanishi wa duru kadhaa za mazungumzo ya amani ambayo hayakuzaa matunda.

XS
SM
MD
LG