Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon yuko nchini Burundi kwa ziara inayonuia kutatua mzozo ambao umekumba nchini hiyo kwa karibu mwaka mmoja.
Ban aliwasili Bujumbura Jumatatu kabla ya mkutano na viongozi wa kisiasa na asasi za kiraiya.
Ziara hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzuru nchini humo katika juhudi za kuleta suluhu kati ya rais Pierre Nkurunziza na wapinzani wake.
Kabla ya ziara ya katibu mkuu huyo, watu 4 waliuwawa kwenye shambulizi la gruneti kwenye mji mku.
Burundi imekumbwa na ghasia tangu Aprili mwaka uliopita baada ya rais Nkurunziza kushinda kwenye muhula wa tatu ulioleta utata wa kikatiba.
Wafuatiliaji wanahofia ghasia hizo ambazo zimeuwa zaidi ya watu 400 na kuwakosesha wengine 230,000 kutorokea nchi jirani zinaweza kupelekea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi yenye makabila mawili ya Hutu na Tutsi.