Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:49

Katibu Mkuu wa NATO anasema anaimani Marekani itaendelea kuisaidia Ukraine


Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza katika moja ya mikutano mjini Brussels
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza katika moja ya mikutano mjini Brussels

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya siku mbili na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels, Stoltenberg alipongeza kile alichokiita msaada wa kijeshi ambao haujawahi kutokea wa washirika wa NATO ambao wameutoa kwa Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Russia

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg anasema ana imani kuwa Marekani itaendelea kutoa msaada kwa Ukraine huku kukiwa na migawanyiko miongoni mwa wabunge wa Marekani kuhusu kuidhinisha ufadhili zaidi kwa ajili ya juhudi za vita vya Ukraine.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya siku mbili na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels, Stoltenberg alipongeza kile alichokiita msaada wa kijeshi ambao haujawahi kutokea wa washirika wa NATO ambao wameutoa kwa Ukraine katika kukabiliana na uvamizi wa Russia.

Changamoto iliyopo sasa ni kwamba tunahitaji kuendeleza msaada huo”, Stoltenberg alisema. Alielezea uungaji mkono kwa Ukraine kama wajibu wa NATO, akisema kwamba ushindi wa Russia nchini Ukraine itakuwa “janga kwa Wa-ukraine” na hatari kwa wanachama wa NATO.

Forum

XS
SM
MD
LG