Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 00:19

Rais Karzai anaitembelea Marekani


Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo siku ya Jumatano kamanda wa vikosi vya Marekani na NATO, huko Afghanistan Jenerali McChrystal na balozi wa Marekani huko Afghanistan, Karl Eikenberry walikutana White House kutayarisha mazungumzo hayo kati ya viongozi wa Marekani na Afghanistan.

Uhusiano kati ya Marekani na Afghanistan uliharibika baada ya ziara ya Rais Obama huko Afghanistan mwezi Machi, kutokana na tuhuma za Rais karzai wa Afghanistan kwamba nchi za Magharibi zilitaka kuharibu utaratibu wa kuhesabu kura za uchaguzi. Rais Obama alijibu matamshi hayo kwa hasira na kuzusha wasi wasi kwa wiki kadhaa ikiwa Rais Karzai atatembelea tena White House.

Ingawa bw Karzai alijaribu kurekebisha uhusiano kutokana na mzozo alousababisha, lakini majadiliano atakayokua nayo na Rais Obama pamoja na mashauriano na waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary Clinton, pamoja na mikutano ya mawaziri wanaofuatana nae yatakua jaribio jingine la kurudisha uhusiano katika njia nzuri.

Balozi wa Marekani huko Afghanistan Eikenberry alizungumza na waandishi wa habari huko White House alisema, “Kutakuwepo na majadiliano katika siku zinazokuja juu ya masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na njia bora za kutekeleza dhamira za serikali ya Marekani kusaidia kuimarisha haraka taasisi za usalama na mahakama ya Afghanistan”.

Miongoni mwa masuala muhimu yatakayo jadiliwa wakati wa ziara ya siku nne ya Karzai ni masuala yanayohusiana na upatanishi na kuwarudisha katika jamii wapiganaji wa Taliban, juhudi zinazoendelea za Marekani na NATO kujenga kikosi cha polisi na jeshi la Afghahnistan litakalokua na uwezo kamili.

Kufuatana na ratiba iliyopangwa na Rais Obama majeshi ya Marekani yataanza kuondolewa kutoka Afghanistan mwezi Julai mwakani. lakini maafisa wa Marekani wanasisitiza kwamba hakuna tarehe maalum ya kuondolewa wanajeshi wote na kwamba utaratibu wote utategemea na hali ilivyo nchini humo.

XS
SM
MD
LG