Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Somalia lilimaliza kujengwa upya Mwaka 2020, baada ya miongo kadhaa ya vita, uporaji, na kutelekezwa lakini janga la COVID 19 liliahirisha mipango ya onyesho la kwanza hadi sasa.
Maonyesho ya kwanza ya jumba hilo la makumbusho tangu kufungwa na kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991 yalifunguliwa Julai 15 kwa michoro,picha na sanamu za wasanii 18 kutoka Somalia na nje ya nchi.
Wasanii wa kigeni ikiwa ni pamoja na wale kutoka Italia, Mexico, na Sweden walionyesha kazi zao kwa mbali kutokana na masuala ya usafiri na usalama.
Kwa Wasomali wengi kama Sumayo Abdi mwenye umri wa miaka 24 hii ilikuwa mara yao ya kwanza kutembelea makumbusho yao ya kitaifa anasema
“kila mtu ambaye amefika kwenye maonyesho haya ana furaha sana kwa sababu yanawakilisha urithi wetu na urithi wa mama na mababu zetu” anasema Sumayo.
Mkurugenzi wa makumbusho Osman Geedoow alisimamia urejeshwaji wa jumba hilo la makumbusho lililoanzishwa mwaka 1933 na anasema wako tayari kulirudisha katika ukuu wake wa zamani.
Jumba la makumbusho limeanza kazi yake na hatua inayofuata itakuwa ni kuweka vitu vya kitamaduni kwenye jumba hili la makumbusho. Kwa vile jumba hili la makumbusho lina jengo la ghorofa nne kwa sasa linafanya kazi kwenye ghorofa ya chini na ghorofa ya pili. Ghorofa mbili zilizobaki za jengo ni tupu. Mbili zilizobaki zinapaswa kujazwa hadi vitu vya kitamaduni kwani vinawakilisha utamaduni na historia ya Kisomali”anaongeza Osman Geedoow wa Makumbusho ya Taifa.
Mkuu wa Chuo cha Kitaifa cha Utamaduni cha Somalia Abdulkadir Hussein anabainisha kuwa vitu vingi viliporwa wakati wa miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kauli mbiu ya maonyesho ya kwanza ya jumba la makumbusho inaitwa Hoy ambayo inamaanisha nyumbani kwa lugha ya Kisomali.
Waziri wa Elimu na Utamaduni wa Somalia Farah Sheikh Abdulkadir alitaja maonyesho haya ya kwanza katika miongo kadhaa kuwa hatua muhimu na ishara ya kuboreshwa kwa usalama na utulivu.
Wakati Somalia bado inakabiliwa na mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab onyesho hili la kwanza katika jumba la makumbusho lililojengwa upya la mji mkuu linapelekea hali ya kawaida na utulivu inayohitajika sana.
Maonyesho haya ya sanaa yataendelea katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Somalia kwa muda wa miezi sita.
Forum