Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:42

Jeshi la Pakistan lauwa wanamgambo karibu na mpaka wa Afghanistan


Wanajeshi wa Pakistan wakishika doria kwenye wilaya ya Wazirstan ambako wanamgambo waliwawa. Picha ya maktaba.
Wanajeshi wa Pakistan wakishika doria kwenye wilaya ya Wazirstan ambako wanamgambo waliwawa. Picha ya maktaba.

Jeshi la Pakistan limesema Jumamosi  kwamba limeshambulia maficho ya ‘magaidi’  kwenye eneo tete  karibu na mpaka wa Afghanistan na kuuwa wanamgambo watano wakati wa mapambano ya risasi.

Shambulizi hilo kulingana na habari za kiintelijensia, lilifanyika usiku kucha katika wilaya ya kaskazini ya Waziristan kwenye jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, na pia limemuua kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo hao, anayehusika na mashambulizi kwa vikosi vya usalama, chombo cha habari cha jeshi kimesema.

Jeshi halijataja jina la kundi hilo, lakini lile la uasi la Tehrik I Taliban Pakistan, au TTP limesema kwamba maficho yao yalivamiwa na kuthibitisha kuuwawa kwa wapiganaji wake wanne. Taarifa ya kundi hilo iliyotumwa kwa wanahabari pia imedai kwamba kulikuwa na mauaji makubwa kwa upande wa vikosi vya kijeshi vilivyofanya uvamizi.

Idara ya kupambana na ugaidi ya jimbo hilo kwenye ripoti yake ya mwaka iliyotolewa Ijumaa, imesema kwamba mashambulizi kutoka kwa wanamgambo katika jimbo la Khyber Pakhtunkwa yameua maafisa 185 wa polisi na kujeruhi wengine 400 mwaka huu.

Ripoti hiyo imediai kuwa majeshi ya usalama kwa upande wao wamewaua wanamgambo 300 na kukamata wengine zaidi ya 900 ndani ya kipindi hicho.

Forum

XS
SM
MD
LG