Kikosi Kazi cha Pamoja cha Kanda cha Tume ya Ziwa Chad kinasema watoto kadhaa waliokolewa mwaka jana katika operesheni dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu. Mamlaka ya Cameroon inafanya kazi kuwatafuta wazazi wa watoto hao.Kikos Kazi hicho maarufu MNJTF, kinasema watoto watano walikabidhiwa kwa maafisa wa Cameroon siku ua Alhamisi baada ya kuokolewa na wanajeshi wa Chad.
Kikosi kazi kimesema wanajeshi wa Chad waliwagundua wavuala watano katika eneo tete la Ziwa Chad, wakionekana wachafu, wenye njaa na wagonjwa.Kamanda wa kikosi, Meja Jenerali Abdul Kalifa Ibrahim kutoka Nigeria, alisema vijana hao walikaa kwa miezi kadhaa katika utumwa chini ya Boko Haram. Alisema alipozungumza na kituo cha taifa cha utangazaji cha Cameroon CRTV. “Ilikuwa bahati mbaya walitekwa na Boko Haram, lakini waliweza kukimbia.
Wanajeshi wa Chad waligundua kuwa ni watoto wa Cameroon. Tutafanya operesheni zaidi. Matumaini yetu ni kwa Boko Haram kujitokeza na kusema hii imetosha,” aliongezea kamanda Ibrahim. Cameroon inasema watoto 25 kati ya 60 walihamishwa kutoka nchini na jeshi la pamoja katika muda wa wiki tatu zilizopita, ama waliokolewa wakati wa operesheni za kijeshi au walikimbia kutoka kwenye kambi za Boko Haram na kujisalimisha kwa wanajeshi kutoka Cameroon, Chad na Nigeria ambao wanapambana wana jihadi. Serikali inasema watoto hao ni kati ya umri kuanzia miaka 9 mpaka 19.