Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:21

Jens Stoltenberg anaitaka Kosovo kupunguza mivutano na Serbia


Jens Stoltenberg, mkuu wa NATO akiwa katika mojawapo ya mikutano ya NATO huko Brussels
Jens Stoltenberg, mkuu wa NATO akiwa katika mojawapo ya mikutano ya NATO huko Brussels

Stoltenberg raia wa Norway na katibu mkuu wa muungano wa kijeshi, alisema amezungumza na mkuu wa sera za mambo ya nje  wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell kuhusu Kosovo na kwamba Pristina na Belgrade lazima wajihusishe katika mazungumzo yanayoongozwa na EU.

Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg siku ya Jumapili ameitaka Kosovo kupunguza mivutano na Serbia, siku mbili baada ya mapambano kati ya polisi wa Kosovo na waandamanaji ambao wanawapinga mameya wa Albania kuchukua madaraka katika maeneo ya kikabila ya Serbia.

Stoltenberg raia wa Norway na katibu mkuu wa muungano wa kijeshi, alisema amezungumza na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, kuhusu Kosovo na kwamba Pristina na Belgrade lazima wajihusishe katika mazungumzo yanayoongozwa na EU.

Pristina lazima iache kueneza na siyo kuchukua hatua za upande mmoja, za kuyumbisha, Stoltenberg alisema katika ujumbe wa Twitter.

Wa-serbia ambao ndio wakaazi wengi katika mkoa wa kaskazini huko Kosovo, hawakubali tamko la 2008 la uhuru kutoka Serbia na bado wanaiona Belgrade kama mji mkuu wao, zaidi ya miongo miwili baada ya vita kumalizika mwaka 1999.

Watu wa kabila la Albania ni zaidi ya asilimia 90 ya wakaazi wa Kosovo kwa ujumla.

Wa-serbia walikataa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Aprili na wagombea wa Albania walishinda katika manispaa zote nne, kwa asilimia 3.5 ya waliojitokeza.

Wa-serbia wa eneo hilo wakiungwa mkono na Belgrade, walisema hawatawakubali mameya hao na kwamba siyo wawakilishi wao.

Siku ya Ijumaa, mameya watatu kati ya wanne walisindikizwa katika ofisi zao na polisi, ambao walitupiwa mawe na kisha polisi walijibu kwa kutumia gesi ya kutpa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji.

Polisi walikuwa na silaha na magari ya kivita walikuwa bado wanalinda ofisi za mameya siku ya Jumapili.

Taarifa ya pamoja kutoka balozi za Marekani, Italy, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, umoja unajulikana kama kundi la Quint, na ofisi ya EU huko Pristina wali-ionya Kosovo dhidi ya hatua yoyote nyingine yoyote ya kulazimisha fursa ya kuingia kwenye majengo ya manispaa.

Forum

XS
SM
MD
LG