Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:58

Jean Pierre Bemba asema yeye ndio mgombea bora wa upinzani.


Makamu rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels, July 24, 2018.
Makamu rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels, July 24, 2018.

Mbabe wa zamani kivita na aliyewahi kuwa makamu rais katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba amesema Jumanne kwamba anaamini anaweza kuwa mgombea bora kuwakilisha upinzani mwezi Desemba katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais lakini akasema yuko pia tayari kumuunga mkono mgombea mwingine .

Katika mahojiano yake ya kwanza ya kina mbele ya umma tangu kuachiwa huru mwezi Mei baada ya kukata rufaa juu ya hukumu yake ya uhalifu wa kivita huko The Hague, Bemba aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba kugombea urais si jambo analong’ang’ania lakini akajigamba kwa uzoefu wake na sifa za uongozi alizonazo. Kujiandikisha kugombea urais kunafunguliwa rasmi Jumatano.

Rais Joseph Kabila ambaye ameongoza tangu 2001 anazuiwa na muda wa mihula kuweza kugombea tena lakini amekataa kusema mbele ya umma kama hatagombea tena.

XS
SM
MD
LG