Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:18

Jaja Bashengezi mwanamuziki wa Congo Washington Dc aeleza harakati za kusaidia nchi yake.


Jaja Bashengezi
Jaja Bashengezi

Jaja Bashengezi au Papa Jolly ni mwanamuziki mzaliwa wa Mashariki mwa Congo na ana kipaji cha muziki akipiga muziki wake kwa kujifunza na kupata uzoefu kutoka kwa wanamuziki wengine hakwenda shule yeyote ya muziki kujifunza kupiga vyombo bali amejifunza mwenyewe.

Akizungumza na jukwaa la Vijana la Sauti ya Amerika Jaja alijikuta akiwa mkimbizi baada ya ghasia kuikumba familia yake zinazoendelea huko mashariki mwa Congo na hatimaye alifika Marekani.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:51 0:00

Akiwa ni mkazi wa jiji la Washington Dc kwa sasa anasema anapiga muziki ukiwa ni sehemu ya maisha yake akisema “upo kwenye damu”.

Jaja anasema yeye anapiga muziki wa asili na ni mwanaharakati pia wa haki za watu wa Congo akiwa ametoa albam yake mpya iitwayo Ndule katika lugha ya Lingala ikiwa na maana ya Muziki, ambao ni wa asilia si kama muziki uliozoeleka wa Congo wa aina ya Soukouss.

XS
SM
MD
LG