Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 20, 2025 Local time: 23:47

Ivory Coast yaingia fainali kwa kuifunga DRC 3-1


Kikosi cha Ivory Coast kinachoingia fainali ya kombe la mataifa Afrika 2015
Kikosi cha Ivory Coast kinachoingia fainali ya kombe la mataifa Afrika 2015

Ivory Coast imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la mataifa barani Afrika kwa mara ya tatu katika muda wa miaka tisa baada ya ushindi wa kishindo wa 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC Jumatano mjini Bata.

Yaya Toure alifungua lango kwa mkwaji mkali kutoka nje ya penalti box katikati ya kipindi cha kwanza lakini dakika chache baadaye Dieumerci Mbokani aliipatia DRC bao la kusawazisha kwa njia ya penalti baada ya mlinzi wa Ivory Coast kuunawa mpira.

Muda mfupi kabla ya halftime kwenye dakika ya 40 mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Gervinho aliipatia timu yake bao la pili kwa njia ya kichwa baada ya pasi kutoka kwa Wilfried Bony.

Ivory Coast walijihakikishia ushindi katika dakika ya 67 kwa goli la Willfried Kanon kwa kuusukuma tu mpira kwa goti karibu kabisa na lango la DRC.

Ivory Coast sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili Alhamisi kati ya wenyeji Equatorial Guinea na Ghana, wakati DRC itacheza katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu atakayeshindwa katika mechi ya Equatorial Guinea na Ghana.

Fainali ya kombe la mataifa Afrika mwaka huu itachezwa Jumapili Februari 8.

XS
SM
MD
LG