Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja nchini Syria, Israel imefanya mamia ya mashambulizi nchini humo, ikilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon, pamoja na jeshi la Syria.
Chombo cha habari cha serikali ya Syria, SANA, kimesema kwamba mfumo wake wa ulinzi wa anga umenasa makombora kadhaa kwenye anga ya Damascus, akiashiria mashambulizi kutoka Israel. Hata hivyo awali chombo hicho kiliripoti sauti ya mlipuko karibu na Damascus.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights linalofuatilia mapigano nchini humo limesema kwamba silaha za Israel zimekuwa zikilenga kituo cha Iran kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus.