Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:06

Israel yaongeza mashambulizi kwenye mji wa Gaza wa Khan Younis


Moshi ukipaa juu ya mji wa Khan Younis kufuatia mashambulizi ya Israel. Jumamosi Desemba 30, 2023.
Moshi ukipaa juu ya mji wa Khan Younis kufuatia mashambulizi ya Israel. Jumamosi Desemba 30, 2023.

Israel inaendelea na mashambulizi yake huko Gaza, ikiushambulia mji wa kusini wa Khan Younis  usiku kucha kwa mashambulizi ya mabomu ya angani pamoja na vifaru.

Ripoti zinasema kampeni kali sana zinafanyika wakati jeshi likitarajia kuingia mjini humo wakati wowote. Shirika la habari la AFP limesema kwamba mmoja wa wanahabari wake ameripoti kusikia mfululizo wa makombora kwenye miji ya Khan Younis na Rafah.

Mji wa Rafah uko karibu na mpaka wa Misri, ambako maelfu ya wapalestina walitafuta hifadhi kutokana na mapigano yanayoendelea. Ripoti zimeongeza kusema Irael imefanya mashambulizi ya anga kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat na katikati mwa Gaza na kuvunja maeneo mawili ya Hamas huko Beit Lahia kaskazini mwa Gaza.

Ripoti za mashambulizi kadhaa huko Gaza zimetolewa baada ya maafisa wa afya kusema kwamba karibu watu 200 wameuwawa ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita. Umoja wa Mataifa umeshutumu kile ilichokiita Israel hivi karibuni kuulenga msafara wa misaada wa magari ya misaada kwenda Gaza kulikofanywa na vikosi vya Israel.

Thomas White mkurugenzi wa shirika la UN, la UNRWA linaloshugulikia wakimbizi wa Palestina, alisema Ijumaa kupitia ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba wanajeshi wa Israel waliushambulia msafara wa magari ya misaada kaskazini mwa Gaza, kwenye njia ambayo ilitengwa na jeshi la Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG