Mkuu wa ujasusi wa Israel anatarajiwa kuongoza mazungumzo ya sitisho la mapigano na wapatanishi ambayo yanaanza tena nchini Qatar siku ya Jumapili kujibu moja kwa moja pendekezo jipya kutoka kwa Hamas, chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kimeliambia shirika la habari la Reuters leo Jumamosi.
Mazungumzo kati ya kiongozi wa Mossad David Barnea, Waziri Mkuu wa Qatar na maafisa wa Misri yataangazia mianya iliyosalia kati ya Israel na Hamas ikiwa ni pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa na misaada ya kibinadamu, chanzo kimesema.
Israel ilisema Ijumaa kuwa itatuma ujumbe wake mjini Doha, lakini haikueleza ni lini itafanya hivyo au nani atashiriki. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alitarajiwa kuitisha mkutano wa baraza la mawaziri la usalama kabla ya mazungumzo hayo.
Maafisa wa Israel hawakupatikana mara moja kutoa maoni yao siku ya Jumamosi, ni siku ya Sabato ya Wayahudi.
Forum