Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:54

Iraq yatangaza kupambana na Islamic State


Waziri mkuu wa Iraqi Minister Haider al-Abadi
Waziri mkuu wa Iraqi Minister Haider al-Abadi

Muungano wa vikosi vya wanamgambo na wanajeshi wa serikali ya Iraq wameanza mashambulizi makali kuwaondoa wanamgambo wa Islamic State nje ya mji wa Tikrit.

Waziri mkuu na amiri jeshi mkuu wa Iraq, Haider Al-Abadi, ametangaza kuanza kwa oparesheni Jumapili wakati akisafiri mji wa jirani wa Samarra.

Safari ya bwana Abadi, ni ya kuangalia juhudi za kuokoa mji wa Tikrit na jimbo la jirani la Saladin.

Bwana Abadi, amewataka wapiganaji wa kabila la Sunni kuachana na kundi la Islamic State.

Amewapa kile kilichoitwa nafasi ya mwisho kwa wapiganaji wa kabila la ki-Sunni na kuwaahidi kutoa msamaha wakati wa mkutano na wanahabari mjini Samarra.

Maelfu ya wanamgambo wa Kishia, Kikabila, na vikosi vya Iraq inadaiwa wameungana kuupigania mji huo.

Afisa wa zamaji wa mji huo aliiambia Sauti ya Amerika kwamba kutakuwa wanatarajia mapambano makali.

XS
SM
MD
LG