Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:12

Iran inasema imeendelea na mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani ya nyuklia


Mfano wa mitambo ya nyuklia ya Iran
Mfano wa mitambo ya nyuklia ya Iran

Program ya nyuklia ya Iran kwa muda mrefu imekuwa chini ya uchunguzi kutoka kwa mataifa ya magharibi na kusababisha vikwazo ambavyo vimeathiri uchumi wa nchi hiyo

Iran imesema siku ya Jumatatu kuwa imeendelea na mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kupitia utawala wa Sultani wa Oman kuhusu mkataba wake wa nyuklia na uwezekano wa kubadilishana wafungwa.

Program ya nyuklia ya Iran kwa muda mrefu imekuwa chini ya uchunguzi kutoka kwa mataifa ya magharibi na kusababisha vikwazo ambavyo vimeathiri uchumi wa nchi hiyo. Makubaliano ya mwaka 2015 yaliipa Tehran nafuu ya vikwazo vinavyohitajika kwa kubadilishana na vikwazo vya program yake ya nyuklia kabla ya kubatilishwa na Marekani kujiondoa mwaka 2018.

Katika siku za karibuni, miji hiyo miwili imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba walikuwa karibu kufikia makubaliano ya mpito kuchukua nafasi ya makubaliano ya mwaka 2015. Tunakaribisha juhudi za maafisa wa Oman na tulibadilishana ujumbe na chama kingine kupitia mpatanishi huyu juu ya kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Nasser Kanani alisema Jumatatu.

Hatujawahi kusitisha michakato ya kidiplomasia, aliongeza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa kila wiki, akisisitiza kuwa mazungumzo hayakuwa ya siri. Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Washington uliharibika mwaka 1980 kufuatia mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 yaliyoongozwa na kiongozi wa kwanza wa Iran, Ayatollah Ruhollah Khomeini. Juhudi za kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 hadi sasa zimeshindwa kutoa matokeo.

Forum

XS
SM
MD
LG