Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:02

Idara ya taifa ya Uhalifu Uingereza imeokoa zaidi ya dola milioni 23 zilizoibiwa Nigeria


Dikteta wa zamani wa kijeshi wa Nigeria Sani Abacha.
Dikteta wa zamani wa kijeshi wa Nigeria Sani Abacha.

Idara ya taifa ya Uingereza ya uhalifu NCA, imeokoa zaidi ya dola milioni 23 zilizoibiwa kutoka  Nigeria na dikteta wa zamani wa kijeshi marehemu Sani Abacha.

Idara ya taifa ya Uingereza ya uhalifu NCA, imeokoa zaidi ya dola milioni 23 zilizoibiwa kutoka Nigeria na dikteta wa zamani wa kijeshi marehemu Sani Abacha, imeeleza Alhamisi, ikiwa ni tukio la karibuni la mfululizo wa kuokoa fedha kama hizo kote duniani.

Abacha alitawala taifa la Nigeria lenye idadi kubwa ya watu na mzalishaji mkubwa wa mafuta Afrika kuanzia mwaka 1993 mpaka alipofariki dunia mwaka 1998, kipindi ambacho aliiba mpaka dola bilioni 5 za fedha za umma kwa mujibu wa shirika la Transparency International, na hakufunguliwa mashitaka.

Fedha hizo zilizookolewa ni sehemu ya fedha zilizofichuliwa na wizara ya sheria ya Marekani.

XS
SM
MD
LG