Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:37

Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mapigano imevuka watu 25,000


Moshi ukifuka huko Gaza baada ya mashambulizi Januari 18,2024.
Moshi ukifuka huko Gaza baada ya mashambulizi Januari 18,2024.

Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mapigano ya zaidi ya miezi mitatu nchini Israel imevuka watu 25,000, Wizara ya Afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas ilisema Jumapili.

Wizara hiyo ilisema idadi ya vifo ni 25,102, wakiwemo raia na wapiganaji wa Hamas, na takriban asilimia 70 ni wanawake na watoto. Maafisa wa afya walisema watu 62,681 wamejeruhiwa katika mzozo huo.

Katika muda wa saa 24 zilizopita, wizara hiyo ilisema kuwa Wapalestina 178 wameuawa na 293 wamejeruhiwa.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Grant Shapps aliiambia Sky News Jumapili kwamba inasikitisha kusikia upinzani wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa taifa la Palestina wakati vita vya Israel na Hama vitakapomalizika.

Forum

XS
SM
MD
LG