Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:36

Idadi ya vifo nchini Madagascar kutokana na kimbunga Freddy imeongezeka

Sehemu ya paa ya jengo huku Kimbunga Freddy kikipiga Trou-aux-Biches, Mauritius, Februari 20, 2023.REUTERS
Sehemu ya paa ya jengo huku Kimbunga Freddy kikipiga Trou-aux-Biches, Mauritius, Februari 20, 2023.REUTERS

Idadi ya vifo nchini Madagascar kutokana na kimbunga Freddy imeongezeka hadi watu wanne, serikali ilisema Jumatano, wakati dhoruba hiyo ikielekea magharibi katika taifa la kisiwa kuelekea zaidi kwenye bara la Afrika.

Kimbunga Freddy kilipiga kusini-mashariki mwa Madagascar Jumanne jioni kikiwa na upepo mkali wa hadi kilomita 180 kwa saa na kilisababisha kufurika kwa eneo hilo na kuezua paa za nyumba. Kimbunga hiki kilipiga karibu mwezi mmoja baada ya dhoruba Cheneso kuua watu 33 na kuwalazimisha maelfu kuhama makazi yao huko Madagascar.

Katika taarifa, Ofisi ya Kitaifa ya Hatari na Majanga ya serikali ilirekebisha idadi ya waliokufa hadi wanne kutoka kwa mmoja hapo awali. Dhoruba hiyo imesababisha watu 11,047 kuyahama makazi yao, ilisababisha mafuriko katika nyumba 2,276 na kuharibu nyingine 2,267, ilisema.

Dhoruba hiyo inaweza kuathiri zaidi ya watu milioni 3.3 kwa jumla nchini Msumbiji, Madagascar na Zimbabwe, OCHA ilisema, ikinukuu tathmini ya Mpango wa Chakula Duniani.

XS
SM
MD
LG