Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:47

Human Rights watch yahimiza Guinea kutenda haki


Jeshi la Guinea likifanya doria kwenye mji wa Conakry.
Jeshi la Guinea likifanya doria kwenye mji wa Conakry.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linahimiza Guinea kuhakikisha kunatendwa haki kwenye kesi ya wanaume na watoto wa kiume waliokamatwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi.

Zaidi ya watoto na wanaume 125 waliokamatwa wakati wa mapambano baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili Novemba 7. Matokeo hayo yalimpatia ushindi kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Alpha Konde.

Mapambano hayo yalikuwa kati ya makundi ya makabila hasimu wafuasi wa kabila la Peuhl la waziri mkuu wa zamani Cellou Diallo na kabila la Malinke la kiongozi wa upinzani Alpha Konde.

Msemaji wa Human Rights Watch yenye makao yake hapa Marekani, Bi. Corinne Dufka anasema wengi wa wafungwa hao wanashikiliwa kwa sababu za kikabila au kisiasa.

Bi Dufka anasema kwamba waliokamatwa wanadai kuwa vikosi vya usalama vinawaomba fedha ili kuweza kuwaachilia huru.

XS
SM
MD
LG