Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:35
VOA Direct Packages

Hofu yaendelea kutanda Iran kutokana na mashambulizi ya sumu kwenye shule za wasichana


Baadhi ya wasichana wa shule wa Iran wakiwa hospitalini baada ya kupewa sumu.
Baadhi ya wasichana wa shule wa Iran wakiwa hospitalini baada ya kupewa sumu.

Idhaa ya Persia ya Sauti ya Amerika imesema Jumatano kwamba mashambulizi ya gesi yenye kemikali yanaendelea nchini Iran, na hasa kwenye shule za wasichana, katika miji kadhaa ukiwemo Tehran, huku darzeni ya wanafunzi wakilazwa hospitalini.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopewa VOA, pamoja na video za mitandaoni, takriban shule 5 kwenye mikoa tofauti ya Iran zimeshambuliwa kwa gesi yenye kemikali. Mashambulizi hayo ya sumu yalianza kwenye shule za wasichana Novemba 30 mwaka jana kwenye mji wa Qom, na hatimaye kuenea kwenye sehemu nyingine za nchi.

Kati kati ya mwezi Machi, chombo cha habari cha serikali ya Iran kiliripoti kwamba zaidi ya wasichana 1,200 kutoka takriban shule 60 walikua wanaugua kutokana na kupewa sumu. Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini humo wanasema kwamba idadi hiyo huenda ikazidi wanafunzi 7,000.

Jumanne shirika la Amnesty International lilionya kuwa haki za masomo, afya na maisha ya mamilioni ya wasichana wa shule yalikuwa hatarini kutokana na mashambulizi hayo ya gesi yenye kemikali, yanayolenga shule za Iran.

XS
SM
MD
LG