Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 12:56

Hazina yatahadharisha iwapo Marekani itashindwa kulipa deni lake la Taifa Juni 1


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amewaita viongozi wa bunge wiki ijayo khuko White House kujaribu kutatua mzozo wa upande mmoja kuhusu ukomo wa deni.

Biden anawaita viongozi wote wanne wa vyama vyote katika baraza la wawakillisha na seneti kukaa pamoja kwa majadiliano.

Hatua hiyo inakuja baada ya Wizara ya Fedha kuonya kuwa serikali inaweza kushindwa baadhi ya bili zake mapema mwezi Juni ikiwa bunge halitaongeza kikomo cha mkopo.

Mswaada uliopitishwa na warepublican katika Baraza la Wawakilishi wiki jana kuongeza ukomo wa deni ni pamoja na kupunguza matumizi makubwa ambayo baraza la Seneti linalodhibitiwa na Wademokrat ilisema haitaidhinisha.

White House imesisitiza kuhusu kuongezwa kwa kiwango hicho deni bila masharti yoyote.

Biden alisema atafanya mashauriano tu kuhusu kupunguza bajeti baada ya kiwango kipya cha ukomo wa deni kuwekwa.

Waziri wa Fedha Janet Yellen na watalaamu wengine wa sera wameitaka Washington kuondoa kiwango, wakisema kinapelekea urasimu katika maamuizi ambayo tayari yamefanywa.

Yellen alionya kwamba kushindwa kulipa deni mwezi Juni huenda "kukachochea janga la kiuchumi na kifedha."

Hata hivyo, kiwango cha deni kinaugnwa mkono na wote Wademocrat na Warepublican, na vyama vyote viwili vimetumia fursa wakati chama kimojawapo hakina udhibiti wa White House.

XS
SM
MD
LG