Viwango vya juu vya joto viliikumba Ugiriki siku ya Jumanne wakati wafanyakazi wa zima moto walipopambana na moto wa msituni katika kisiwa cha Rhodes na maeneo mengine nchini humo.
Moto huo umedumu kwa zaidi ya wiki moja na huu wa Jumanne ni pamoja na moto katika kisiwa cha Evia na Corfu. Mamlaka nchini humo zimewahamisha zaidi ya watu 20,000 kutoka Rhodes, wengi wao wakiwa watalii, pamoja na zaidi ya watu 2,000 kutoka Corfu.
Kikosi cha zimamoto cha Ugiriki kinasaidiwa na wafanyakazi wa zima moto kutoka nchini Uturuki, Israel, Misri na Umoja wa Ulaya.
Watabiri wa hali ya hewa walitarajia kuwepo siku kadhaa zaidi za joto la kiwango cha juu kabla msimu wa mapumziko ya joto kuwasili.
Forum