Alitoa maoni hayo Jumamosi katika mkutano na wanahabari uliofanyika baada ya ufunguzi wa Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa.Guterres alieleza kwamba kwasababu ya ukosefu wa msaada wa kifedha, bara la Afrika linakabiliwa na hali ngumu sana.
Akiongea katika mkutano wa wanahabari uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu Antonio Guterres alisema ili kuonyesha uwezo wa bara hilo, mfululizo wa changamoto lazima kwanza zishughulikiwe.
“Mufmo wa fedha usiofanya kazi na usio wa haki unazinyima nchi nyingi za kiafrika ahueni ya madeni na masharti nafuu ya ufadhili wanayohitaji. Mifumo na miundo, kuanzia afrika na elimu mpaka hifadhi ya jamii, uanzishaji wa nafasi za ajira na usawa wa jinsia haupatia uwekezaji kwasababu wa ukosefu wa msaada,” amesema Guterres.
Guterres alizungumzia athari ya madeni ambayo yako kwenye uchumi wa bara hilo katika matamshi yake mapema siku hiyo katika sherehe za ufunguzi wa mkutano wa kilele wa AU. Alisisitiza kwamba kuziendeleza nchi za Afrika mara nyingi kunaachwa wakati wakopeshaji wa kimataifa waweke mipango yao wa kifedh
Ameongeza kusema kwamba nchi za Afrika haziwezi kuwekeza katika maeneo haya muhimu sana au kupanda ngazi ya maendeleo huku zikiwa zimefungwa kamba nyuma.
Guterres ameelezea kwamba Afrika kikawaida haina uwakilishi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katika taasisi ya Bretton Woods.