Kampuni hiyo ilisema kwamba hali hiyo ilisababishwa na kukatwa tena kwa mitandao ya kimataifa iliyokuwa imerejeshwa awali. Gaza ilishuhudia kukatwa kwa huduma za mawasiliano kwa siku mbili kuanzia Ijumaa iliyopita, hali iliyoacha wakazi takriban milioni 2.3 wakiwa bila mawasiliano na ulimwengu, hali iliyoathiri upelekaji wa misaada inayohitajika.
Ukosefu wa sasa kwa huduma za simu na internet umetokea saa chache baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kwenye kambi ya wakimbizi katika mji wa kazkazini mwa Gaza wa Jabaliya, yaliyosababisha vifo vya takriban watu 50, na wengine 150 kujeruhiwa, kulingana na wizara ya afya ya Palestina.
Msemaji wa jeshi la Israel amethibitsha shambulizi hilo kwa kituo cha televisheni cha CNN, akiongeza kwamba kamanda wa ngazi ya juu wa Hamas alikuwa kwenye eneo hilo. Taarifa ya baadaye kutoka jeshi la Israel la IDF, imemtambulisha afisa huyo kama Ibrahim Biari, akisemekana kuwa kiongozi wa shambulizi mbaya lililofanywa na wanamgambo wa Hamas, Oktoba 7 nchini Israel.
Forum