Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema wamekamilisa kuwakagua watu zaidi ya 100 waliokamatwa mwishoni mwa juma kwenye bahari hindi, na imetambua kwamba walikuwa ni raia wa Tanzania pamoja na wakenya kadhaa.
Wakuu wa Usalama kutoka eneo hilo wamesema japo wengi wao ni wavuvi kutoka Pemba, waliokuwa wakivua nyakati za usiku, watafunguliwa mashitaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria na kuchukuliwa kama wahamiaji wasio na hati zinaozhitajika.
Watu hao wote ambao ni wanaume walikamatwa kwa sababu za kiusalama kulingana na mkuu wa idara ya polisi katika county ya Mombasa, Francis Wanjohi ambae pia amesema kuwa uchunguzi uaonyesha kuwa walikuwa wavuvi. Hata hivyo amesema idara ya uhamiaji na ile ya uvuvi zitachukua hatua za kisheria dhidi ya washukiwa hao.