Mkuu wa EU Josep Borell alisema mapema wiki iliyopita kwamba suala la kushikiliwa kwa Johan Floderus lilikuwa limezungumziwa mara kadhaa na taifa hilo la Kiislamu.
Kupitia tovuti maalum, familia yake, marafiki pamoja na wafuasi wa Floderus wanaomba hatua ya haraka ya kimataifa ya kuachiliwa kwake mara moja, na kurejeshwa Ulaya salama, wakati anapoadhimisha miaka 33 tangu kuzaliwa.
Walisema kwamba Floredus ameshikiliwa bila kufunguliwa mashitaka yoyote kwenye jela ya Evin mjini Tehran, ambako wafungwa kwa kisiasa pamoja na wale waliokamatwa kutokana na masuala ya kiusalama wakiwemo raia wa Iran wamefungwa.
Familia yake imesema kwamba Floderus alizuru kote Mashariki ya Kati akisomea lugha za watu tofauti pamoja na maeneo ya kihistoria, wakati pia akisaidia kwenye miradi ya kibinadamu nchini Iran kwa niaba ya EU. Alikamatwa Aprili 2022 pale alipokuwa karibu kuondoka nchini humo.
Forum