Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:50

Familia ya Rusesabagina ina wasiwasi na afya yake


Paul Rusesabagina, alipongezwa kwa ushuja katika filamu ya Hollywood kuhusu auaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994. Anakabiliwa na kesi nchini Rwanda.
Paul Rusesabagina, alipongezwa kwa ushuja katika filamu ya Hollywood kuhusu auaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994. Anakabiliwa na kesi nchini Rwanda.

Familia ya Paul Rusesabagina, anayezuiliwa katika jela nchini Rwanda kwa tuhuma za ugaidi inaelezea kuwa na wasiwasi wake juu ya hali yake ya afya.

Familia inaomba Rusesabagina aruhusiwe kupewa madaktari kutoka nje ya nchi ili wamuhudumie.

Rusesabagina alifikishwa mahakamani kwa ya mara kwanza Jumatatu, kiowa ni wiki moja na nusu baada ya kukamatwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, katika mazingira ya kutatanisha.

Binti yake Carine Kanimba, katika maohojiano na Sauti ya Amerika amesema kwamba baba yake alionekana ni mwenye afya dhaifu alipokuwa kizimbani.

Familia yake imeiomba serekali ya Rwanda kumruhusu daktari kutoka nje ya nchi amchunguze hali yake ya afya yake na apate huduma anazohitaji.

“Tumepata taarifa kwamba ni hawampi dawa zake anazotumia, kuna dawa anazotakiwa kutumia kila siku. Lakini sasa tumeambiwa anapewa dawa asizozijua, na ambazo hata sisi hatuzijui. Kwa hiyo, tunaiomba Rwanda ikubali daktari wetu aje kumuhudumia." alisema Carine.

Familia ya Rusesabagina, inaeleza pia haina imani na mawakili aliopewa Rusesabagina autoka chama cha mawakili Rwanda, ili wamtetee katika kesi inayomkabili.

Inaomba atetewe na mawakili watakaopendekezwa na familia.

“Kusema kwamba amepewa mawakili wa kumtetea ni ujanja mtupu. Kwa sababu mawakili hao wenyewe hawakutufahamisha kama baba atafikishwa mahakamani. Huu ni ujanja kudai kuwa ana mawakili wanaomtetea, wakati hawakutupa taarifa yoyote kuhusu kufikishwa kwake mahakamani. Hii ni ishara kwamba nchini Rwanda, hakuna utawala wa sheria.” alisema binti wa Rusesabagina.

Rusesabagina alipata umaarufu kutokana na filamu iliyoelezea maisha yake mwaka 2004, ikielezea namna alivyowaokoa watu zaidi ya 1200 katika mauaji ya halaiki.

Filamu hiyo ilimfanya rais wa zamani wa marekani George W Bush, kumpa Rusesabagina tuzo ya ushujaa.

Lakini baadhi ya manusura wa mauaji ya halaiki na rais wa Rwanda, Paul Kagame, waliendelea kusema kwamba Rusesabagina, alitumia filamu hiyo kwa maslahi ya kibiashara.

Hivi karibuni Rais Kagame, alisema Rusesabagina anafuatiliwa na vyombo vya sheria vya Rwanda, kutokana na vitendo vya kuhatarisha usalama wa taifa kupitia kundi analolifadhili la FLN.

Lakini familia yake inaendelea kukanusha madai hayo dhidi ya Rusesabagina.

Alhamisi makahama ya mwanzo mjini Kigali, inatarajiwa kutoa maamuzi iwapo Rusesabagina ataachiwa kwa dhamana au la.

XS
SM
MD
LG