Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:24

Evans Chebet ashinda Boston Marathon, Obiri ashinda kwa wanawake Kipchoge akosa medali

Evans Chebet wa Kenya (kushoto) na Hellen Obiri pia wa Kenya (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la mshindi baada ya ushindi wa kila mmoja kwa wanaume na wanawake katika mbio za Boston 2023.( Picha na Eric Canha-USA TODAY Sports)

Mwanariadha wa Kenya Evans Chebet alitetea tena  taji lake la Boston Marathon wakati Mkenya mwenzake Hellen Obiri alishinda mbio hizo kwa upande wa  wanawake siku ya Jumatatu lakini mpinzani wao na bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge alimaliza katika nafasi ya sita.

Muda wa Chebet wa saa mbili dakika tano na sekunde 54 ulikuwa sekunde 10 na mkimbiaji wa Tanzania Gabriel Geay ambaye alishika nafasi ya pili huku Mkenya Benson Kipruto bingwa wa mwaka 2021 akishika nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 6.

Chebet, ambaye pia alishinda New York mwaka jana, alishika kasi baada ya umbali wa kilomita 35 lakini Geay alikataa kushindwa kirahisi na Kipruto alishika kasi kwa kilomita 40 na kufanya mbio hizo kuwa za watu watatu.

Lakini ikiwa imesalia maili moja Chebet alikuwa amejitengenezea uongozi usioweza kupingwa na alikuwa peke yake alipovuka mstari wa kumalizia na huku akishangiliwa na umati akiwa mtu wa kwanza tangu mwaka 2008 kutetea taji lake la Boston.

Mshikiliaji wa rekodi ya dunia Eliud Kipchoge alikuwa miongoni mwa vivutio vikubwa katika Mbio hizo za Marathon za Dunia lakini alipoteza kasi yake karibu na nusu ya mchuani huo na kupitwa na wenzanke na hatimaye kumaliza katika nafasi ya sita.

Akikimbia mbio zake za pili za marathon, Obiri alikimbia bega kwa bega na kundi la waongozaji lililojaa kwa wingi karibu muda wote mbio wote wa mbio hizo kabla ya kuwaacha ikiwa imesalia maili moja na kushinda kwa muda wa saa 2 dakika 21 na sekunde 38 kwa kelele huku akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Boston.

XS
SM
MD
LG