Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Ron Godard anasema kura ya Umoja wa mataifa kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Cuba haitasaidia kusogeza mambo mbele. Jumuiya ya kimataifa ilipiga kura karibu kwa kauli moja jana Jumanne ili kumaliza miaka 50 ya vikwazo vya kiuchumi na kibiashara dhidi ya Cuba.
Wanachama 199 wa baraza kuu la umoja wa mataifa wameitaka Washington kumaliza hatua hizi zilizowekwa wakati wa kilele cha vita baridi.
Marekani na Israel ndio nchi pekee zilizopinga azimio hilo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Umoja huo kuonesha ungaji mkono mkubwa namna hiyo kutaka kukomeshwa kwa vikwazo hivyo tangu ilipoanza kuzungumzia suala hilo kwa miaka 24 mfululizo.
Balozi Godard amesema, “Ni jambo la kusikitisha kwamba licha ya kuonyesha maendeleo ya pande mbili serikali ya Cuba imechagua kuwasilisha azimio ambalo linafanana na yale ambayo yaliwasilishwa katika miaka ya nyuma. Na alisisitiza kwamba Marekani, hata hivyo haitabanwa na historia ya kutokuaminiana.
Lakini waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodriguez Parrilla ameihimiza Marekani kuondowa vikwazo akisema ni kwa maslahi ya kitaifa ya Marekani kufanya hivyo.
Alisema “Tuna tumaini kwamba bunge la Congress la Marekani litachukua hatua kubadilia sera hii, mbaya na katili iliyotumika siku za nyuma na kuchukua maamuzi yalio na mrengo wa hisia na thamani ya raia wake.”
Godard aliliambia baraza hilo kwamba kurudisha uhusiano kamili na Cuba, marekani imetekeleza hatua kadhaa za kihistoria zilizolengqwa kuanzisha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili.
Amesema tangu Desemba wakati mahusiano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba amefanya mambo kadhaa ya kihistoria yaliopangwa kuanza kuweka sawa mahusiano ya pande mbili.
Ifikapo mwisho wa mwaka Goddard anasema tunatarajia kutangaza mambo kadhaa tuliyofanikisha ambayo yatawanufaisha watu wetu wote kwa pamoja.