Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:00

Marekani kupunguza silaha za nuklia


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton ameuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa unao tathmini mkataba wa kutoeneza silaha za nuklia, kwamba, Marekani inadhamira ya kuzuia kuenea na kuangamiza silaha za nuklia pamoja na kutangaza idadi ya silaha zake za nuklia.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Bi Hillary Clinton alisema rais Barack Obama amefanya kupunguza kitisho kinachotokana na silaha za nuklia kua kipaumbele cha sera ya kigeni ya Marekani. Alisema hii ilianza na hotuba yake ya Prague mwaka jana na kuimarishwa na mkataba wa START ulotiwa sini hivi karibuni na Rashia na tathmini mpya ya msimamo wa nuklia wa utawala wa Obama inayopinga kutengenezwa silaha mpya za nuklia za Maraekani.

Bi Clinton aliwambia wajumbe kwamba marekani itaendelea kutafuta njia mpya za kupunguza akiba yake ya nuklia na itaimarisha hali ya kua na uwazi zaidi kuhusiana na silaha zake za atomiki, kwa kutangaza idadi ya silaha za nuklia ilizonazo na ni ngapi ilizoangamiza tangu 1991.
“Kwa hivyo kwa wale wenye shaka ikiwa Marekani itatekeleza sehemu yake ya kuangamiza silaha, basi hii ndiyo rikodi yetu, hii ni dhamira yetu na inapeleka ujumbe wa wazi”.

Pentagon ilitangaza takwimu za hadi 1992, zinazonesha Marekani ina akiba ya silaha za nuklia zenye vichwa 5 113. Hapo 1967 wakati wa vita baridi Marekani ilikua na vichwa elfu 31.

Waziri Clinton alitangaza kwamba Marekani itatoa dola milioni 50 kwa kipindi cha miaka mitano kwa mradi mpya wa matumizi ya amani ya Idara ya Kimataifa ya Nishati ya Atomiki, wenye lengo la kusaidia mataifa kutengeneza vinu vya nuklia vyenye usalama kwa ajili ya matumizi ya kiraia.

XS
SM
MD
LG