Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 20:44

China imeanza kuwakaribisha wawakilishi wa nchi 130 kwa mkutano wa BRI


Rais wa China, Xi Jinping ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa Belt and Road Initiative (BRI)
Rais wa China, Xi Jinping ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa Belt and Road Initiative (BRI)

Viongozi wameanza kuwasili katika mji mkuu wa China kwa ajili ya tukio la kuadhimisha muongo mmoja wa BRI, mradi muhimu wa Rais Xi Jinping ili kuongeza ushawishi  wa China duniani

China imeanza kuwakaribisha wawakilishi wa nchi 130 kwa mkutano ambao utagubikwa na vita vya Israel na Hamas wakati Beijing ikizidi kuombwa kusaidia ghasia zisisambae.

Juu kabisa kwenye orodha ya mwaliko katika jukwaa la Belt and Road Initiative (BRI) la China, ni Rais wa Russia Vladimir Putin, katika ziara yake ya kwanza yenye nguvu kubwa ya ulimwengu tangu uvamizi wa Ukraine ambapo utawala wake umetengwa kimataifa.

Viongozi wameanza kuwasili katika mji mkuu wa China kwa ajili ya tukio la kuadhimisha muongo mmoja wa BRI, mradi muhimu wa Rais Xi Jinping ili kuongeza ushawishi wa China duniani.

Wakati China ina matumaini kuwa mkutano huo utasaidia kuimarisha msimamo wake kimataifa, vita vya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas vitaendelea kugonga vichwa vya habari.

Israel ilitangaza vita dhidi ya kundi hilo la Kiislamu baada ya msururu wa wapiganaji wake kuvuka ulinzi mkali hapo Oktoba 7, na kuwapiga risasi, kuwachoma visu, na kuwachoma moto hadi kufa zaidi ya watu 1,400 wengi wao raia.

Zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makaazi yao kufuatia hali ya machafuko na kukata tamaa kutokana na mashambulizi makali ya Israel katika Ukanda wa Gaza inayodhibitiwa na Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG